005Msamaha6.4jan62017

005Msamaha6.4jan62017                                   Msamaha.                                                          192

Msamaha, Hasira, Chuki, Upendo, Makwazo, Kisa.
View 01.

-->Swala la Msamaha, ni lazima kuzungumziwa katika nafsi moja, wewe kama wewe, mimi kama mimi, yeye kama yeye,   maana kwa upande wa mtu zaidi ya mmoja, au nafsi zaidi ya moja mf:- Jamii, kanisa, darasa, taifa  (nchi), familia, swala la msamaha, hasira, upendo, na makwazo ni jambo ambalo haliwezi kutolewa maelezo ya uhakika.
-->Ni kwakuwa siku ile ya mwisho ni kwa nafsi moja ndo kupongezwa au hukumu. Na kwakuwa hukumu, ni kwa matendo, japo msamaha na upendo, ni kutoka moyoni, basi, uoneshe na uonyeshe. Yawezekana upo katika kundi fulani na kufanyiwa jambo fulani ambalo limewaudhi kama kundi (kanisa, darasa, shule, wanafunzi, waalimu, jamii, n.k) msamaha utoke kwako/ndani yako wewe kama wewe wala si kutoka kwa mtu mwingine/watu wengine.
- ->Samehe wewe kama wewe. Usiwaangalie wengine. Hatakama yeye ni kiongozi. Tena, ukiwaangalia hao wengine, iwe ni kwa kusudi la kuwashawishi wasamehe (nao wasamehe). Achana na mambo ya Dunia. Yesu asema, usipowasamehe unakuwa kama watu wa Dunia, Math 5:43- 48.  Je, unadhani kutokusamehe kunatokana na Mungu?!.
Math 5:43- 48,
43 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;   44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,   45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. 46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? 47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? 48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

-->Tazama utakosa Ufalme wa Mbinguni kwa Kutokusamehe! Hata kama wewe ni mtumishi wa Mungu (na ulitoa pepo kwa jina lake). Hatakama taifa lako limewaka hasira dhidi ya taifa lingine au dini yako (dhehebu) ipo katika majonzi na hasira kutokana na uovu mliotendewa na dini nyingine /dhehebu lingine, hebu, wewe kama wewe, simama imara usamehe maovu yote uliyotendewa/ mliyotendewa. Ukifunga/ukiweka kisa, ni jambo baya sana na kama hutosamehe utahukumiwa. Na bila ya kumsamehe ni vigumu sana kuenda kumuhubiria.            --> Kisa cha nini ewe Mkristo unayemwamini Yesu Kristo aliyekuambia usamehe mara7 mara 70 wewe usisamehe?!. Math 6:15 – Msipo wasamehe wengine, Mungu naye, kamwe hatowasamehe/hatokusamehe.

Math 6:15, 15 ‘Bali msipowasamehe watu makosa yao,
wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu’.
Mathayo 18: 21 Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?   22 Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.

Uovu aliokufanyia mtu yawezekana unalingana na uliomfanyia Mungu. Mf, uzinzi. Wewe umezini bila mwenzi kujua, lakini mwenzi alipozini wewe ulijua, wewe unamwomba Mungu akusamehe, afu humsamehi mwenzi. KAMWE HUTOKUWA NA AMANI PAMOJA NAYE. Mwenzio kamtenda makosa Mungu, ndambi yake ni yake, lakini, na wewe pia amekukosea. Basi, Samehe. Ili na wengine wajifunze mema kutoka kwako maana nawe umemkosea Mungu ijapokuwa wengine/mwenzi hajajua. Bila hivyo, nawe hutosamehewa.
->Wasababishao makwazo wapo tu. Makwazo hayana budi kutokea, lakini ole ni kwa yeye ayasababishaye au kwa wewe uyasababishae - Luka 17:1.

Luka 17: 1 Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake! 2 Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa. 3 Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe.   4 Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.

Je, wewe umeshawahi kusababisha makwazo?!. NB: Inategemea ni makwazo gani, maana unapomwambia asiye Mkristo halisi (kuna Wakristo jina) twende kanisani, kwake ni kwazo lakini kwa Mungu si kwazo. Yesu alipokuta biashara inafanyika katika hekalu, akaamua kuharibu vilivyomo kule, ilimaanisha alikuwa kikwazo kwa wafanya biashara, NA KWAZO HILO, HALIKUWA KWA ALIYEMTUMA. Mwili wako ni hekalu la Kristo, kama Bwana akikuta hakuna ibada humo, atavuruga yote ufanyayo (kwa wakati na sababu). Hapo ndo utakwazika. Je, utasemaje juu ya Yesu?!. Utamfungia kisa Yesu au mtumishi/watumishi wake? - kwakuwa amekuambia jema ambalo haliendani nawe?!.

Hivi, unajua kuwa:-

.i. Kumkasirikia mwanadamu umemkasirikia Mungu?!.
.ii. Kumtendea wema mwanadamu umemtendea wema Mungu?!.
.iii. Kumkataa mwanadamu umemkataa Mungu?!.
.iv. Kutokumsaidia mwanadamu hujamsaidia Mungu?!.
   Soma kwa kina na kwa makini, Mathayo 25: 34 - 51.

Mathayo 25: 34 - 51,
34 Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia.   35 Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.   36 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.  
37 Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.   38 Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,   39 wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.   40 Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;   41 wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.  
42 Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.   43 Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.  
44 Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.  
45 Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake?   46 Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo.   47 Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote.  
48 Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; 49 akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi;  50 bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua,  
51 atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga men o.

-->Kwenda mbinguni ni hiari, ila ukitaka kwenda kuna mambo ya lazima ya kufanya. Moja wapo ni KUSAMEHE.

Yesu ndiye njia *ata Shetani anajua*, yeye asema, usamehe. Sasa wasubiri nini?!. Mbinguni hawakutani watu wenye kinyongo pamoja!?.
Je, wadhani ni akina nani watakao sema, “Tulitoa pepo kwa Jina lako ”, ila Mungu atawaambia, ‘siwajui ninyi kwa wema, nawajua kama watenda maovu’. “Ondokeni kwangu ninyi watenda Maovu”.
                Luka 13:23-30,
23 Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,   24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.   25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;   26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.  
27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.  
28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje.   29 Nao watakuja watu toka mashariki na magharibi, na toka kaskazini na kusini, nao wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu.   30 Na tazama, wako walio wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, na wa kwanza watakaokuwa wa mwisho.
Maovu hayo ni pamoja na Kutokusamehe. Je, unakubali kabisa kuenda Jehanamu, kisa tu hukusamehe?!. Aibu!. Japo umeshinda dhambi ya uzinzi ambayo huwaangusha wengi, ila umeshindwa kumsamehe yule aliyekuwa!?   *mzazi, mpenzi, ndugu, rafiki*?!.

·          Chuki ni uovu. Kama hujamsamehe mtu maana yake una-chuki naye.
·          Je, kusamehe ni lazima au ombi?!.  Au ombi la mkubwa ni sheria yaani ni lazima?!.
·          Jua ya kuwa ni lazima!(Si Ombi). Ni Lazima kusamehe ili uende Mbinguni (kwa wanaotaka kwenda Mbinguni kwa kumaanisha tu)!.
·          Je, Mbinguni kuna watu ambao wana bifu?!.
·          Je, ili uishi kwa furaha na amani na watu, usamehe au laa?!.
-->Swali. Je, ukisamehe unapaswa kusahau?!. 

->Ninaamini kuwa, Mungu hakumpa Mwanadamu ufahamu wa kusahau mambo yote, kwa sababu mbalimbali mojawapo ni kwaajili ya ushuhuda na kuwafundisha wengine. Ukisahau, maana yake huna ushuhuda. Kama ulishawahi kufanyiwa au kufanya jambo kubwa baya sana hasa kutoka kwa yule ambaye hukumtarajia *kubakwa hasa na mzazi au yeyote, au kuzini na mzazi, shemeji au rafiki wa mpenzi wako au ushoga, kuchomewa nyumba, kutapeliwa na ndugu wakaribu sana au wa mbali*, huwezi kusahau kamwe. Mpaka siku ya mwisho ukimwona utasema huyu alinifanyiaga jambo fulani, ila nilimsamehe/nimemsamehe.

Mambo ya kusahau huwa ni madogo tu. Na kama mtu akizungumzia juu ya jambo kubwa, ni lazima utalikumbuka tu.
o    Je, inawezekana kwa binadamu mwenye akili timamu kutokusamehe mtu afu kusema ati ‘nampenda’?!.   au
o    Je, inawezekana kutokumsamehe mtu afu kusema ‘sina chuki nae/naye’?!.
Unapenda mambo mazuri au mabaya?!.
·          Je, wadhani, kama hujamsamehe mtu, ni wazo gani jema utakaloliwaza juu yake?!.
·          Je, kusamehe ni jambo jema?!.
·          Kama ni jema, je, wewe upo tayari kufanya jambo jema? (sasa/kwa wakati) au kinyume cha jambo jema au kulichelewesha jambo jema?!.

-->Hasira zipo, ila:-

.i. Usiwe mwepesi wa hasira (kuwa kama Yesu).
.ii. Uwe na hasira kidogo, maana kwa hilo, utafanya jambo jema, pia utamwonesha alokosea alofanya ni makosa sana si kumchekea mtu anayechelewesha maendeleo ya kiimani + anapokuwa amehari. NB: Upole kiasi pia (Gal5:22) maana kila kitu ni kwa kiasi.  Gal 5:19 – Hasira ni jambo la mwili (baya).
-          Waefeso 4: 26 Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; 27 wala msimpe Ibilisi nafasi.
-          Tito 1:7kiongozi asiwe mwepesi wa hasira.
-          Yako 1:20 – Hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu.
-          Mathayo 5:24 – Yesu asema, usitoe sadaka yako, kabla hujapatana na uliyekwazana naye.

Mwanadamu amemkosea Mungu, je wewe?. Wewe uliyekutana naye muda mchache tu, umemkuta amekosana na wazazi wake ambao walimlea, sasa sembuse akikuosea wewe?!.
Ukimsamehe mtu utakuwa na uwezo wa kutambua sauti ya Mungu kupitia watu. Maana kama hujamsamehe, ata Mungu akimtuma kwako utaishia kumsikiliza na kumpuuzia. Kwa kupuuzia maneno aliyoyasema juu yako unakuwa umempuuzia Mungu.

-          Ni Vyema kusamehe kutokako moyoni kukatoka ulimini kwa kutamka.
-          Mungu anataka tusameheane ndugu. Maana kunafaida nyingi ata kwa akili timamu tu, bila kutumia Biblia kuelimishana na kukumbushana (kwa walioshaelimika).
-          Wewe ndo unasamehe/unamsamehe ila si yeye kukusamehe wewe. Yeye kutokukusamehe wewe yawezekana ukachangia, ila vyema ukaangalia kwa upande wako zaidi--<- Kwa maana, Kutokusamehe kwake, si dhambi kwako. Ila  Angalia usimkwaze Shetani afu ukamwomba msamaha. Angalia, umkwazaposhetani, usimwombe msamaha. Namaanisha, kuomba msamaha si kwa wote. Namaanisha, unapoambiwa usamehe, na wewe uombe msamaha ili upendo uzidi na chuki ikome hapo ndipo kuishinda hasira. Waweza tumia kauli nyingi kuomba msamaha:- ‘Nisamehe’, ‘Yaishe’, ‘Sitorudia’, ‘Nitakuwa mwaminifu’, ‘Nitajituma’, ‘Sitokubaliana naye/nao tena’, ‘Nitajihahidi’n.k.
-          KUSAMEHE SI KUSAHAU – Kwakuwa/kwa sababu ya kutunza ushuhuda, kusamehe ni kutunza ushuhuda. Na kusahau, si maamuzi.

Unajua kwanini tunasema usamehe?!. Tazama, angalia aliyekukosea ni Mungu.
(kwa mtazamo wako –ata na wengine)?!. Je, unajua kwanini tunasema usamehe?!.
Kusamehe, ni kuonesha upendo. Na ujue kuwa, Upendo:-
1Wakor 13 : Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na
upatu uvumao.2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha
kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;  5   haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;  6   haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
8   Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika”.
Je, wajua kuwa sababu zako/yako za/ya kutokusamehe si njema?!. Ndiyo ni sababu ila unapaswa kujua kuwa...

Sababu za kutokusamehe:-
Ila jua ya kuwa:-
Sababu za kusamehe.
NB: zote ni za lazima.
.1. Kujihesabia haki/ kuona kuwa unastahili, kutokana na madai halali (mf: ya madeni) yako/haki yako kwa uliyekoseana naye/nao.
à Haki unayoihesabia/unayojihesabia, yawezekana ikawa si haki mbele za Mungu. Na hatakama ni haki mbele za Mungu, Kusamehe bado kunabaki pale pale.
->Kama ni haki mbele za Mungu, basi, mwachie Mungu. Kwani wewe ulikufa kwaajili ya mtu?!. Je, Yesu hakusema kuwa huku kutakuwa na tabu?!. ‘Watu watateswa kwa jina langu’?!
->Je, wewe ndo unaye hukumu?! Ya Mungu, mwachie Mungu. Yako ni yapi wakati wewe ni mali ya Mungu?!.
->Je, wadhani kati ya mbinguni na duniani wapi kuna haki?!. Ukijua kuwa huku hakuna haki, usishangae unapokosa haki, na kuwa tayari kwa kukosa haki.
Math 5:6 Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa. 10 Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao 20 Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni
44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,  45  ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.’.
-> Kuonesha + Kuonyesha kuwa unamwamini Yesu, maana yeye ni mwenye haki na si wanadamu tena si huku duniani.
.2. Kiburi + hasira kwa kujiona bora dhidi ya m-baya wako na kumwona hafai/hakukutendea jema.
à Kiburi hakipendezi kwa mtu anayemfuata Kristo. Unamwekea mchungaji wako kiburi, sasa atakuchungaje?.
NB: Mchungaji ni mwalimu, kiongozi (yeyote Yule), Mungu, Padri, n.k. Marko 7:20. Kiburi cha leta unajisi.
->Kuonesha kuwa, hasira iletayo kiburi haimo ndani yako.
Na kuonesha kuwa kiburi huna na unastahili kuenda mbinguni.
.3. Uchungu na maumivu, yatokanayo na ubaya uliotendewa/ uliofanyiwa.

à Kiwango kilekile ambacho wewe mwenyewe umesamehe, ndicho hicho hicho kiwango ambacho Mungu atakusamehea. Tazama, uchungu wakufanya usisamehe kwa wakati au kutokusamehe kabisa, Mungu naye atakufanyia hivyo.    -->Math 6:12,14,15. Uchungu wako umekufanya uwe mgumu kusamehe, Je, unajua umemhuzunisha Mungu kwa mangapi?!.
->Kuonesha kuwa umekubali kukwazwa na waulimwengu kwakuwa ndivyo alivyotabiri Yesu basi unaishi kwa amani.
.4. Kuwafanya watu ni kama Mungu na malaika (kwako) kwa kusema huwa hawakosei.
à Kama unataka kuwa kama Yesu, kwa kuwa mwanafunzi wake/kumfuata yaani Mkristo -> Matendo 11:26 usamehe kama yeye alivyowasamehe wengi (hasa alipokuwa msalabani. Na ujue alikuja kwaajili ya wenye dhambi ambao tunahitaji msamaha. Au unadhani alikuja kwaajili ya watakatifu?!.
->Kukubali kuwa wanadamu si wakamilifu (nikiwemo) basi tutiane moyo na kuonyana kwa upendo. Kuoneshana na kuonyeshana kutawale kati yetu.
.5. Kutokuamini kuwa msamaha unawezekana.
= Kuamini kuwa msamaha hauwezekani.
+ Kuamini kuwa, haiwezekani kusamehewa (na Mungu).
+ Kuamini kuwa nikisema Siwezi kumsamehe ndo inakuwa.
-> Msamaha kama msamaha naoujua mimi ambao ni kutoka moyoni ambao ni lazima uwe na upendo kwa wote, UTASAMEHE TU. Wewe umesema, ‘sitomsamehe’, na utatoa hesabu ya kila neno likutokalo, Math 12:46,47 (siku ya mwisho). Sema, nimekusamehe na utende jambo, hakika utakuwa na amani moyoni.
->Jambo gani analolishindwa BWANA juu ya maisha yako?!. Hebu litaje!?.
->Mbona tumemkosea sana Mungu na kila siku tunashauriwa kumwomba msamaha kabla hata ya shukrani?!.
->Kuonesha kuwa, Mungu hashindwi. Hatakama ulishindwa kusamehe kwa kumpa Shetani nafasi ya kwanza, ila sasa unaweza/umeweza kuonesha kuwa, Mungu wako yu hai na anataka tusameheane.
.6. Kutaka kulipiza kisasi (kwanza au laa) + Kulipiza kisasi.
->Kisasi ni cha Mungu. Waru 12:9, Ebr 10:30, Hasira zako, zinaweza kukufanya ukatenda dhambi. Ata kulipiza kisasi. Kwa Mungu, si vyema.
->Kuonesha kuwa, hasira hainitawali katika kulipiza kisasi na kumwachia Mungu.
.7. Kufuata mkumbo, kuiga, kushawishika,
Kushaurika, kutoshaurika.
Jua, Ni upumbavu huo. ->Ati kwa kuwa fulani hajasamehe, na wewe unagoma kusamehe. NI upumbavu huo. Yeye hakufa kwaajili  ya dhambi zako. (kama Yesu alikufa kwaajili ya dhambi zetu, mbona basi kunahukumu?!.). Mwige Yesu asiyebadilika. Maana huyo ulomwiga leo kwa kusamehe au kwa kutokusamehe kesho asiposamehe je?!. Yesu habadiliki. Kwanini umwige mtu wakati Yesu Yupo?!.
-> Kujihakikishia kuwa, ulikuja duniani mwenyewe na utaikabidhi kazi yako mwenyewe na utapongezwa mwenyewe na hukumu ni mwenyewe.

Math 7:21- Ukifanya mapenzi ya Mungu, wewe kama wewe ndo utaenda mbinguni.

Math 10:32 – Ukimkiri Yesu (wewe binafsi) naye atakukiri.

Math 16:27 – Mtu binafsi atalipwa kwa matendo yake.
.8. Ubishi. Bila kujali ni hasira au laa, kuiga au laa.
Kubishia maandiko wakati umeambiwa kwa wazi kabisa kuwa lazima usamehe.
-Kumbishia Roho Mtakatifu, Mungu, na watumishi wa Mungu.
Je, mpaka sasa unabisha?!.
Wapo waliokuwa na hasira zaidi yako na walisamehe. Wapo walioona maisha ya watu waovu na wema na wakajifunza kuiga mema na kuacha mabaya. Wapo ambao walikuwa wanambishia Roho Mtakatifu, na kuwabishia watumishi wa Mungu lakini sasa hawana ubishi katika Neno la Mungu.
Jua ya kuwa ubishi ufanyike kwa Shetani ila si kwa Mungu.
Mungu ni wa kumwogopa. Mwalimu mkuu wa shule unaanzaanzaje kumbishia? Unasababu gani ya msingi kumbishia Mungu asemapo nawe kupitia maandiko na watumishi wake?!.
Ni lazima kusamehe kumaanisha kuwa wewe si mbishi katika Neno la Mungu. Neno la Mungu li wazi kwamba usipowasamehe watu, nawe hutosamehewa. Leo unatarajia kwenda mbingu ambayo kuna wenye dhambi? Maana yake dhambi ulizotendaga hutosamehewa, utabaki kuishi kwa neema ila mbingu inafikiwa na wenye nguvu.
----> SABABU kuu ya kusamehe ni wewe kuboresha mahusiano yako wewe na Mungu <-----

-- >Luka 1 : 51 Amefanya nguvu kwa mkono wake; Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao;
- -> Math 5: 40 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.  41  Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.  42   Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.   43   Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;   44   lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,   45   ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.   46   Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?   47   Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?   48   Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.-->Waefeso 4:22 mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya;   23   na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu;  24   mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.  25   Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake.  26   Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;   27   wala msimpe Ibilisi nafasi.   28   Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.  29   Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.   30   Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.  31    Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya;   32   tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Kumbukumbu la Torati 32:35 Kisasi ni changu mimi, na kulipa, Wakati itakapoteleza miguu yao; Maana siku ya msiba wao imekaribia, Na mambo yatakayowapata yatafanya haraka.
-->Luka 21:9 “Nanyi mtakaposikia habari za vita na fitina, msitishwe; maana, hayo hayana budi kutukia kwanza, lakini ule mwisho hauji upesi.   10   Kisha aliwaambia, Taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme;    11   kutakuwa na matetemeko makubwa ya nchi; na njaa na tauni mahali mahali; na mambo ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.   12   Lakini, kabla hayo yote hayajatokea, watawakamata na kuwaudhi; watawapeleka mbele ya masinagogi, na kuwaua magerezani, mkipelekwa mbele ya wafalme na maliwali kwa ajili ya jina langu.   13   Na hayo yatakuwa ushuhuda kwenu.   14   Basi, kusudieni mioyoni mwenu, kutofikiri-fikiri kwanza mtakavyojibu;   15   kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga.   16   Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao watawafisha baadhi yenu.  17  Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu.  18   Walakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu.
-- >Marko 7: 20 “Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi.   21 Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,  22   wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.  23 Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi”.
-- >Mathayo 6 : 9 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,  10   Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.  11   Utupe leo riziki yetu.  12   Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.   13   Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]   14   Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. 15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
-->Matendo 11:26 “hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia”.
- ->1Yoh 1:5 Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lo lote hamna ndani yake.  6   Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;   7   bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.   8   Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.   9   Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.   10   Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.
Waebrania 10:30 Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake.
Warumi 12:19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.

Madhara ya kutokusamehe.
Faida za kusamehe.
.1. Ni Dhambi + kujitia hatiani. Ni dhambi kwasababu hujamtii Mungu aliposema usamehe. Marko 11:25.
->Unakuwa na nguvu hata wakati wa kusali kwa kuwa moyo wako haukuhukumu kuwa unadhambi.
.2. Kutokupokea msamaha kwaajili ya makosa yako mwenyewe.
Math 6:15, Marko 11:25.

-- > Wewe mwenyewe kupokea msamaha kwaajili ya makosa yako mwenyewe (Je, vipi kama sina dhambi?!.  Math 6:14.
-> Maana yake, Kuepuka hukumu ya kuto kusamehe, siku ile ya mwisho.
->Kuwa makao ya Kristo na kuwa na uhakika wa kuenda Juu Mbinguni kwa Baba.
.3. Huzuia majibu ya maombi yako kutoka kwa Mungu. -->Wakati umeudhiwa ukiwa umekwisha omba jambo fulani. Katikati vikainuka vikwazo. Hutopokea majibu ya maombi yako. Kama ukipokea majibu maana yake Mungu haangalii utakatifu wako. Ndo maana ukifunga unapaswa kujitenga na watu.
--> Unapokea majibu ya maombi yako kwa hali ya amani na furaha za BWANA na si za wengine. Na NB: Msamaha mzuri ni katika BWANA na si kwa vingine. Umeomba sana, hukujibiwa, ni kwakuwa, hukuwa na utii kwa kutokusamehe. Na Mungu hasikilizi maombi ya wenye dhambi.
.4. Kunakufanya kuwa mtumwa wa Shetani maana umekuwa makao ya pepo wachafu. Upendo huna maana yake, una chuki, hapo, hasira itakuandama, na hutotenda haki ya Mungu kutokana na hasira ya chuki si ya Mungu. Unaombewa sana na kuhamia kanisa jingine ila bado matatizo yapo.
->Unaepuka utumwa wa Shetani. Ata kuwaza kumnywea mtu pombe hakuna bali kuimba kwa furaha.
--> Kusamehe kunakufungua kutoka vifungo vya Shetani. Bila hivyo, utaombewa sana, ila sifuri tu.
-Unatakasika moyoni mwako kwa kusamehe naye Mungu akufungue/atakufungua kutoka vifungo vya Shetani.
.5. Huathiri afya yako. Hakika mawazo yatakuandama. Mtu unaonekana umekaa umetulia ati mpole, kumbe unawaza mabaya ulofanyiwa na kuwaza kulipiza.
->Huimarisha afya yako, kwa maana, ata kwa zaidi ya asilimia kubwa utakuwa huna mawazo ya hovyo. Moyo wako unawaza upendo tu.
.6. Unaonesha ya kuwa, wewe ni wa ulimwengu huu na unanguvu ya kuyashughulikia yako.
->Unawakilisha kuwa umemwachia Yesu.
.7. ->Huvunja mawasiliano mazuri kati yako na jamii. Hatakama umekosana na kaka, mdogo hatokuwa na amani nawe. Umekosana na mke wa jirani, mmewake hawezi kuwa na amani nawe, hatakama unacheka naye, ila huwezijua moyoni. Haiwezekani wewe umchukie mke wangu afu mimi niwe na amani nawe. Nitakuwa nakupenda, ila sitokuwa na amani nawe. Ata kesho ukija kunihubiria sitokuwa na furaha nawe.
+ ->Huhatarisha amani.
->Huboresha mawasiliano baina ya majirani (ndugu au laa) na watu wengine.
Kuwa na ushirikiano katika maisha kwa ujumla.
->Kutokuhofiana mabaya pale mmoja apatapo tatizo.
->Kusaidiana wakati wowote.
->Kuwa na amani kwa watoto wa familia tofauti kuwa pamoja.

.8. Unasababisha wengine wasisamehe.
->Unasababisha wengine wasamehe. .n.k.

--> Ila, Kusamehe si kula naye sahani moja, si kurudisha mahusiano makubwa, si kumwamini ata 60%, si kumruhusu alinde malizako, si kumpa kila ulichonacho, si kumkumbatia, si kukubali kila akuambialo, si kumruhusu atawale  nyumbani mwako, si kumruhusu aishi nawe, si mpaka akuombe msamaha, si mpaka akubali msamaha wako.  Umemsamehe HUWEZIJUA KUWA kama yeye AMEKUSAMEHE moyoni mwake.    
KUSAMEHE NI NJIA YA KUHUBIRI INJILI. 192p.

View 02.

Vuie

-->Swala la Msamaha, ni lazima kuzungumziwa katika nafsi moja, wewe kama wewe, mimi kama mimi, yeye kama yeye,   maana kwa upande wa mtu zaidi ya mmoja, au nafsi zaidi ya moja mf:- Jamii, kanisa, darasa, taifa  (nchi), familia, swala la msamaha, hasira, upendo, na makwazo ni jambo ambalo haliwezi kutolewa maelezo ya uhakika.
-->Ni kwakuwa siku ile ya mwisho ni kwa nafsi moja ndo kupongezwa au hukumu. Na kwakuwa hukumu, ni kwa matendo, japo msamaha na upendo, ni kutoka moyoni, basi, uoneshe na uonyeshe. Yawezekana upo katika kundi fulani na kufanyiwa jambo fulani ambalo limewaudhi kama kundi (kanisa, darasa, shule, wanafunzi, waalimu, jamii, n.k) msamaha utoke kwako/ndani yako wewe kama wewe wala si kutoka kwa mtu mwingine/watu wengine.
- ->Samehe wewe kama wewe. Usiwaangalie wengine. Hatakama yeye ni kiongozi. Tena, ukiwaangalia hao wengine, iwe ni kwa kusudi la kuwashawishi wasamehe (nao wasamehe). Achana na mambo ya Dunia. Yesu asema, usipowasamehe unakuwa kama watu wa Dunia, Math 5:43- 48.  Je, unadhani kutokusamehe kunatokana na Mungu?!.
Math 5:43- 48,
43 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;   44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,   45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. 46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? 47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? 48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
-->Tazama utakosa Ufalme wa Mbinguni kwa Kutokusamehe! Hata kama wewe ni mtumishi wa Mungu (na ulitoa pepo kwa jina lake). Hatakama taifa lako limewaka hasira dhidi ya taifa lingine au dini yako (dhehebu) ipo katika majonzi na hasira kutokana na uovu mliotendewa na dini nyingine /dhehebu lingine, hebu, wewe kama wewe, simama imara usamehe maovu yote uliyotendewa/ mliyotendewa. Ukifunga/ukiweka kisa, ni jambo baya sana na kama hutosamehe utahukumiwa. Na bila ya kumsamehe ni vigumu sana kuenda kumuhubiria.            --> Kisa cha nini ewe Mkristo unayemwamini Yesu Kristo aliyekuambia usamehe mara7 mara 70 wewe usisamehe?!. Math 6:15 – Msipo wasamehe wengine, Mungu naye, kamwe hatowasamehe/hatokusamehe.
Math 6:15, 15 ‘Bali msipowasamehe watu makosa yao,
wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu’.
Mathayo 18: 21 Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?   22 Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.
Uovu aliokufanyia mtu yawezekana unalingana na uliomfanyia Mungu. Mf, uzinzi. Wewe umezini bila mwenzi kujua, lakini mwenzi alipozini wewe ulijua, wewe unamwomba Mungu akusamehe, afu humsamehi mwenzi. KAMWE HUTOKUWA NA AMANI PAMOJA NAYE. Mwenzio kamtenda makosa Mungu, ndambi yake ni yake, lakini, na wewe pia amekukosea. Basi, Samehe. Ili na wengine wajifunze mema kutoka kwako maana nawe umemkosea Mungu ijapokuwa wengine/mwenzi hajajua. Bila hivyo, nawe hutosamehewa.
->Wasababishao makwazo wapo tu. Makwazo hayana budi kutokea, lakini ole ni kwa yeye ayasababishaye au kwa wewe uyasababishae - Luka 17:1.

Luka 17: 1 Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake! 2 Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa. 3 Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe.   4 Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.

Je, wewe umeshawahi kusababisha makwazo?!. NB: Inategemea ni makwazo gani, maana unapomwambia asiye Mkristo halisi (kuna Wakristo jina) twende kanisani, kwake ni kwazo lakini kwa Mungu si kwazo. Yesu alipokuta biashara inafanyika katika hekalu, akaamua kuharibu vilivyomo kule, ilimaanisha alikuwa kikwazo kwa wafanya biashara, NA KWAZO HILO, HALIKUWA KWA ALIYEMTUMA. Mwili wako ni hekalu la Kristo, kama Bwana akikuta hakuna ibada humo, atavuruga yote ufanyayo (kwa wakati na sababu). Hapo ndo utakwazika. Je, utasemaje juu ya Yesu?!. Utamfungia kisa Yesu au mtumishi/watumishi wake? - kwakuwa amekuambia jema ambalo haliendani nawe?!. Hivi, unajua kuwa:-

.i. Kumkasirikia mwanadamu umemkasirikia Mungu?!.
.ii. Kumtendea wema mwanadamu umemtendea wema Mungu?!.
.iii. Kumkataa mwanadamu umemkataa Mungu?!.
.iv. Kutokumsaidia mwanadamu hujamsaidia Mungu?!.
   Soma kwa kina na kwa makini, Mathayo 25: 34 - 51.
Mathayo 25: 34 - 51,
34 Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia.   35 Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.   36 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.  
37 Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.   38 Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,   39 wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.   40 Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;   41 wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.  
42 Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.   43 Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.  
44 Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.  
45 Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake?   46 Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo.   47 Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote.  
48 Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; 49 akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi;  50 bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua,  
51 atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Comments