.4/8.!!!Kuhusu
Yohana mbatizani.!!!
.i/viii. Hakuwa mtu mdogo“†††lakini ni mdogo sana†††”.
Math 11:11 Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa
wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika
ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye.
.ii/viii. Mfalme Herode alimwona Yesu kuwa ni kama
Yohana Mbatizaji.
Math 14:1 Wakati ule mfalme Herode alisikia habari za Yesu,
akawaambia watumishi wake, 2 Huyo ndiye
Yohana Mbatizaji; amefufuka katika wafu; na kwa hiyo nguvu hizo zinatenda
kazi ndani yake.+ Marko6:14.
.iii/viii. Na
yeye Herode ndo ali mwuaga.
Math 14:8 Naye, huku akichochewa na mamaye, akasema, Nipe hapa
katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji. + Marko 6:24.
.iv/viii. Watu wengine pia walimwona Yesu kuwa ni
Yohana Mbatizaji.
Math 16:14 Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji,
wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. + Marko
8:28, Luka 9:19.
.v/viii. Yohana Mbatizaji alionekana kuwa na pepo.
Luka 7:33.
“†††33 Kwa kuwa Yohana Mbatizaji alikuja, hali mkate wala hanywi divai,
nanyi mwasema, Ana pepo. 34 Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa; nanyi
mwasema, Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao watoza ushuru na
wenye dhambi.†††”
.vi/viii. Na huyo Yohana mbatizaji ndiye Eliya.
Math 17: 10 Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, Basi kwa nini
waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza? 11 Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya
yuaja kwanza, naye atatengeneza yote,
12 ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini
wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa
kwao. 13 Ndipo wale wanafunzi
walipofahamu ya kuwa amesema nao habari za Yohana Mbatizaji.
“†††
.1. Wanafunzi wa Yesu hawakujua kama yeye ni
Eliya.
.2. Wanafunzi wa Yesu waliuliza maswali na
hawakujitia ujuaji na kukaa kimya bali walijitia ujuaji kwa kujua kutoka kwa
mjuaji (mwalimu wao) Yesu.
.3. Yesu alikuwa anajibu maswali
aliyoulizwa.
.4. Petro alipomwona (Math 17:4) alimtambua
kuwa ni Eliya ila si kama Yohana Mbatizaji ijapokuwa Eliya alikuwa wa zamani
sana kuliko Yohana Mbatizaji.
.5. Yesu aliwajuza kuhusu walilouliza baada
ya kuuliza, maana nao wasingeliuliza, hata wao wasingelijua kama
waliyemwulizia. †††”
.vii/viii. Yohana kutamka kwa uwazi kuhusu kupinga
ubatizo wa maji.
Math 3:11 Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba;
bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua
viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
==>> Marko 1:8, Luka 3:16, Yohana 1:26.
“†††.viii/viii. Yohana
Mbatizaji hakujitambua kuwa yeye ni Eliya.
Yohana Mbatizaji asema yeye si Eliya.
Yoh 1:
:21 - Yohana alipoulizwa kuhusu kama yeye ni Eliya
amesema, “mimi siye” na aya ya :25.
Maelezo ya aya zingine,
katika Yohana 1:
.01. :18 - Yesu ni Mungu mwana (utatu)
.02. :20 -
Yohana asema yeye si Kristo.
.03. :20 -
Yohana asema yeye si Eliya.
.04. :20 -
Yohana asema yeye si Yesu (nabii yule :27) niweke ___ rejea zingine).
.05. :22 – Watu walimjia Yohana kumwuliza
maswali naye aliwajibu.
.06. :23 - Yohana ni sauti ya mtu aliaye
nyikani.
.07. :23 - BWANA ana njia ambayo ni jukumu lako
mwanadamu kuinyosha.
.08. :23, :27 - Yohana alikuwa anaijua
historia na pia anayathamini maneno ya manabii.
.09. :23, :27 - Neno la Mungu
litatimia/linatimia/li hai.
.10. :23, :27 - Neno la BWANA lina wakati
wake.
.11. :23, :27 - Biblia ilikuwa inasomwa.
.12. :24 - Mafarisayo walikuwa wadadisi.
.13. :25 – Ilifahamika dhahiri kuwa ubatizo
utakuwepo.
.14. :25 - Mafarisayo walifahamu kuwa
mbatizaji ni Kristo au nabii yule au Eliya na si nje ya hapo.
.15. :26 - Yohana asema, 'mimi nabatiza’ si ‘Yesu
kupitia mimi’.
.16. :26 - Mafarisayo walikuwa hawamjui
Kristo wala nabii yule.
.17. :27 - Yesu ndiye ajaye nyuma ya Eliya na
pia inaonesha kuwa Yohana ni Eliya..
Angalia usiwe kama mafarisayo. Wao neno wanalijua lakini
hawamjui aliyesemwa kwenye neno.
Hivyo ndivyo Biblia ime/ilivyomwelezea Yohana.†††”
|
(sehemu hii bado inafanyiwa marekebisho)
|
Lesson Series
|
|
Downloads
|
.1.
|
006Ubtz3.17jan17.1/8
|
Maana ya ubatizo.
|
|
.2.
|
006Ubtz3.17jan17.1/8
|
|
|
.3.
|
006Ubtz3.17jan17.1/8
|
|
|
.4.
|
006Ubtz3.17jan17.1/8
|
|
|
.5.
|
006Ubtz3.17jan17.1/8
|
|
|
.6.
|
006Ubtz3.17jan17.1/8
|
|
|
.7.
|
006Ubtz3.17jan17.1/8
|
|
|
.8.
|
006Ubtz3.17jan17.1/8
|
|
|
.9.
|
Complete Ubatizo 3. (hakuna
bali ipo ubatizo 2 ambayo ni complete, kupata Ubatizo 2 bonya hapa)
|
|
|
Comments
Post a Comment