.2/8..!!!Malumbano
kuhusu ubatizo (kwa maji)!!!.
(bila
kujali ni maji machache au mengi)
Ukitaka kujua hakuna
haja ya kulumbana kuhusu ubatizo wa/kwa maji, jiulize na ujijibu.
Musa, Ayubu, Abramu
(si Abrahamu)/Ibrahimu, Enoko,Eliya, Elisha, n.k. hao ni baadhi ya watumishi
fulani wa Agano la kale. †††Je, walikuwa watumishi wadogo au wakubwa?!...
Je,
walibatizwa?!. Je, kati ya hao,
akinanani walimtokeaga Yesu? mara ngapi (kuonesha wapo hai)?!. Je,
walibatizwa?!.
†††Mathayo 17, Marko 9, Luka 9,
Mathayo 17:
“†††Katika
aya hizo tunaona mengi:-
.1. :1 - Kuna wakati Yesu alijitenga na kubaki
na wanafunzi wake tu.
.2. :3 -
Musa na Eliya kumtokea Yesu.
.3. :4
- Petro alimwona/aliwaona Musa na Eliya.
.4. :4 - Petro aliwatambua Musa na Eliya.
.5. :8 - Musa na Eliya ni watu.
.6. :9
- Hayo yalikuwa ni maono.
.7. :9
- Yesu ni wa mipango katika wakati wa utimilifu.
.8. :9
- Yesu alijua kuwa atafufuka katika wafu; maana yake alijua kuwa atakufa
(Math 16:23-Petro aliona si vyema kufa kwa Yesu, basi Yesu akamwita Petro
‘Shetani’).
.9. :9 - Yesu ni mwana wa Adamu.
.10. :10
– Wanafunzi wa Yesu walikuwa wanafahamu historia ya kale.
.11. :10 – Wanafunzi wa Yesu walikuwa
wanauliza/wanamwuliza Yesu.
.12. :10 – Wanafunzi walitambua/walimtambua
Yesu kuwa yeye si Eliya.
.13. :10 – Wanafunzi hawakutambua kuhusu kuja
kwa Eliya kutatimia lini ila kutatimia kabla ya Yesu/ kutatimia na ndo
atakuja Yesu.
.14. :10 – Wanafunzi walitambua/walimtambua
Yesu kuwa alitabiriwagwa/alitabiriwaga na ndo wakonaye (mwalimu wao).
.15. :10 – Wanafunzi walitambua/walimtambua
Yesu kuwa yeye si Eliya na wakamhoji/wakamuuliza.
.16.
:10 – Yesu alikuwa akiwajibu wanafunzi wake maswali. (kwakuwa Yesu
alikuwa mwalimu wao?).
.17. :10 – Wanafunzi wa Yesu walijua kuwa
Yesu atakuja na ameshakuja na ndo huyo waliyenaye pamoja, ila kabla yake Yesu
kuna ambaye alipaswa kuja/kutangulia. Sasa ndo wanaona kuwa huyu Yesu nikama
amekuja kabla ya aliyetabiriwa. Yaani waliona kama unabii
umepishana/umepingana.
.18. :11
- Yesu hujibu kwa ufasaha kwa kukubali kinachopaswa kukubaliwa.
.19. :11 - Yesu aliijua historia.
.20. :11 - Eliya alikwisha kuja (kurudi) kabla ya
Yesu.
.21. :12 - Labda Eliya alipokuja hakusemaga kuwa
yeye ni Eliya na kwakutokana na hilo, ndo maana walimtenda walivyotaka na pia
wanafunzi hawakujua/hawakumtambua.
.22. :13 - Wanafunzi wa Yesu waerevu sana.
Kuhusu kutokuwepo na ubatizo miaka ile, †††”
Yeye Yohana Mbatizaji, yupo mbinguni au laa?!.
Je, alibatizwa?!. Je, kabla ya Yohana kulikuwa na ubatizo?!. Kama haukuwepo,
waliendaga wapi?!. Au basi hakuna umuhimu wa ubatizo kama bila kubatizwa
unaenda Mbinguni maana imeonekana wameenda mbinguni.
“†††Manabii wa miaka ile:-
.1. Isaya. .2. Yeremia. .3. Musa. .4. Miriamu.
.5. Debora n.k. Walibatizwa?!...
Wafalme:-
.1. Samweli. .2. Sauli. .3. Sedekia. .4.
Daudi. .5. Sulemani n.k, je, walibatizwa?!...
Bila kujali ni maji mengi au kidogo au
machache au makubwa, je, walibatizwa?!...
Kama hawakubatizwa na Mungu alikuwa pamoja nao
na aliwatumia, Je, si kwako / kwetu?!... au wewe unataka ubatizwe tu na Mungu
asiwe nawe au uwe na Mungu bila
kubatizwa au vyote?!...
Kwa kufikia hapo, sioni haja ya kugombana
kuhusu kiasi au kiwango cha maji ila kuhusu maji ujue kuwa Yesu ni maji
yaliyohai.
-->Mtu anajitetea kwa kusema, ‘hao sawa hawakubatizwa,
ila Yesu alibatizwa’.
Sawa.
Sasa hao pia walioa ila Yesu hakuoa. Hao pia hawakusali kanisani, Yesu naye
hakusali kanisani basi na wewe usisali kanisani. Hao pia hawakutumia Biblia
ya agano jipya na Yesu pia, basi na wewe pia. Hao pia … Umechagua unaloweza
ukalifanya kwa kuliiga na kulifanya, basi sawa, unashangaa kwangu nikichukua
linalonifaa na kulifanya?!...
Sioni haja ya kulumbana.
Kama unahoja zaidi wasiliana nasi/nami. †††”
|
Comments
Post a Comment