Ubatizo kwa maana ya ki-biblia 006Ubtz3.17jan17.1.8.!!!

.1/8..!!!Ubatizo kwa maana ya ki-biblia!!!.

Ubatizo kwa maana ya kibiblia.

Hakuna maana ya moja kwa moja iliyotolewa (kwa uwazi).  Anayejua maana aseme/atuambie/aniambie.
--->Kusema ubatizo wa maji mengi au machache vyote ni sawa si kweli.

Na hatakama ni sawa, Ukweli ni kwamba kubatizwa ni kwa Roho Mtakatifu na ndo kwa moto kwa ushahidi wa andiko/kimaandiko.

Huyo aliyembatizaga Yesu haikuwa kazi yake. Wewe unayebatiza leo ni kazi yako hiyo?!. Wewe uliyebatizwa, aliyekubatiza ni kazi yake?!.

Wewe unayesema maji mengi au machache toa maandiko. Usiwe mtu unaye kariri ya watu na si ya Mungu.
Kwa Mtu anasema Yesu alibatizwa maji mengi.

->Hakuna uhakika kuwa maji ni mengi au laa
(yaliyotumika kumbatizia/kumbatiza).
Eti kisa ni mtoni. Kwani mtoni haiwezekani maji machache/kidogo/ya kichwa?!.

Au kama ni ya kichwa wangelifanyia nyumbani ee?! haya, ila Yeye Yesu hakusema Ubatizwe maji mengi na isitoshe usimwige kila kitu ila msikilize kila kitu.

NB: Kuna tofauti kati ya kusikiliza na kuiga. Ukimwiga Yesu, si mbaya. Ila unamwigaje?.

Kama unamwiga Yesu kwakuwa alibatizwa, basi iga na haya.      
.i. Usioe (kwa mwanaume), kwa wakike sijui mimi.  
.ii. Usiende shule,  
.iii. Usisali kanisani n.k maana yote hakufanya.       
.iv. Usikubali/usiwe mwanafunzi bali wewe ndo uwe mwalimu na uwe na wanafunzi (sasa sijui wao itakuaje maana nao kama wanamfata Yesu hawatakiwi wawe na mwalimu).  
.v. Yesu alitumia sana kauli za 'Mimi nasema', na wewe tumia hizo kauli.   n.k <--- Huko ndo kuiga.


Ila, kama unaiga machache, maana yake unaiga yale unayoyaweza wewe. Basi usiwalazimishe watu waige/wamwige pia. Pia, kama ni kwakuwa ulipenda wewe ndo ukaiga, usiwalazimishe wengine wapende.
Na kama hawatopenda kuiga usiwahukumu. Kama Yesu amesema iga hili, sawa. Ila kama hakusema, usimlaumu mtu na usijione kuwa wewe ni bora sana.
Kuiga so tatizo, ila inategemea unaiganini ili nini.

Umeambiwa ubatizwe kwa maji yoyote?!. Wapi alisema. Au una/mna msingizia Mungu?!.
Mtu asiibuke na hoja zake bila maandiko.

Yesu amesema/ametuambia/aliwaambia katika Mathayo 28:19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;.

Sasa anayesema ubatizwe kwa jina lake ndo umwige?!. Yeye Yesu alibatizwa kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu?!. Haya tufanye kama umemwiga, utabatizwa kwa maji mengi. Je, utatumia jina la nani?!. Kama utatumia lake, sasa umebatizwa kwa jina au kwa maji?!. au kwa maji na kwa jina?!. kama ni kwa maji na kwa jina, umemwiga au umefanya yako?!.
Yeye amesema (Yeye, Yeye, Yeye Yesu amesema) Math 28:19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
Hapo hajasema ata neno moja kuhusu kutumia maji yoyote/yeyote.

“†††
Kwa mujibu wa Math 28:19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
Ubatizo ni kitendo/tendo linalofanywa kwa kutumia jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu na wanafunzi wa Yesu kwa mataifa ili kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi wake Yesu.
NB: Kwa mujibu wa Mathayo 28:19 ni kwa mujibu wa Yesu. †††”


















 (bado kuna marekebisho)




Lesson Series

Downloads
.1.
006Ubtz3.17jan17.1/8
Maana ya ubatizo.

.2.
006Ubtz3.17jan17.1/8


.3.
006Ubtz3.17jan17.1/8


.4.
006Ubtz3.17jan17.1/8


.5.
006Ubtz3.17jan17.1/8


.6.
006Ubtz3.17jan17.1/8


.7.
006Ubtz3.17jan17.1/8


.8.
006Ubtz3.17jan17.1/8


.9.
Complete Ubatizo 3.   (hakuna bali ipo ubatizo 2 ambayo ni complete, kupata Ubatizo 2 bonya hapa)




Comments