Neno la Kila Siku Bread of today Neno la Leo




Daily Bread? (Neno la Kila siku?)



S/N
Verse
Word
1
2
3
4
Isaya 9:6a
[6]Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto mwanamume;
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
5
Kumbukumbu la Torati 11:26-28
[26]Angalieni, nawawekea mbele yenu hivi leo baraka na laana;
[27]baraka ni hapo mtakapoyasikiza maagizo ya BWANA, Mungu wenu, niwaagizayo leo;
[28]na laana ni hapo msiposikiza maagizo ya BWANA, Mungu wenu, mkikengeuka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua.
6
Ukristo katika Biblia.

Matendo ya Mitume 11:26
[26]'c'
Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.

Ni Mara ya kwanza kabisa kuitwa '.....'.
7
Hesabu 6:24-26
[24]BWANA akubarikie, na kukulinda;
[25]BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili;
[26]BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani.
8
Kutoka 1:12
[12]Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli.
9
Panua Mahali pa:-
1. Biashara yako 2019
2. Uchumi wako 2019
3. Elimu yako 2019
4. Upendo wako 2019
5. ...

Ni wewe ndo ufanye, so Mungu akufanyie.

Isaya 54:2.
10
Ufunuo wa Yohana 21:1
[1]Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapanak bahari tena.



Kuna muda:-
 Utapita na vyake.

 Kuna vitu ambavyo lazima viondoke ndo vije vingine.
11
Mathayo 11:28
[28]Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
12
13
Moja ya sifa za Biblia ni:- Kujibu.

Zaburi 119:9

a-Jinsi gani kijana aisafishe njia yake?

Jibu:
b-Kwa kutii, akilifuata neno lako.

Je, Unaswali?.
14
Yakobo 1:12
Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.

Tafakari kushinda majaribu.





15
Waefeso 3:20
[20]Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;
16
Yakobo 4:7-8
[7]Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
[8]Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.
17
Yakobo 4:13-16
[13]Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida;

[14]walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka.

[15]Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi.

[16]Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya.

18
Neno la Leo.

Yoshua 24:15

A-Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia;

B-kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao;

C-lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA.

Amin.
19

"Usipende usingizi usije ukawa maskini; ..."

Mithali 20:13'A.

Ni moja ya sifa ya Biblia kuwa, Inashauri.

Nakutakia usiku mwema.
20
"Kila siku, Bwana hutuhurumia."

Maombolezo 3:22-23

[22]Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii,
Kwa kuwa rehema zake hazikomi.
[23]Ni mpya kila siku asubuhi;
Uaminifu wako ni mkuu.

Jua, kila siku, Bwana ameshatuandilia fungu jema, "rehema".

Amina.




Comments